Tambua haki na wajibu wako ili uweze kupiga kura – Haki Maendeleo

Zoezi la utoaji wa elimu ya mpiga kura Manzese sokoni

Zoezi hili la utoaji wa elimu lilifanyikja kwa njia ya elimu shirikishi na wananchi walipata fursa ya kuuliza maswali pakoja na kuelezea uzoefu wao na changamoto walizowahi kuzipitia.

“Ndugu Mwalusako ameiomba Tume iangalie uwezekano wa madereva wa magari ya Mizigo kuwa na nafasi ya kupiga kura popote ili waweze kutumia haki yao kikatiba “

Maeneo yaliyotembelewa ni pamoja na Buguruni, Manzese Darajani, Soko la Mahakama ya ndizi na Mwembe chai.

Elimu iliyotolewa ni haki na wajibu wa mpiga kura, na wananchi wapoiga kura walisisitizwa umuhimu wa kuzingatiia sheria na taratibu zilizowekwa na Tume ya Uchaguzi ambayo ndio inaratibu zoezi zima la kupiga kura.

EneoWanawakeWanaumeJumla
Buguruni  – Ilala81321
Manzese Darajani, -Ubungo01818
Soko la Mahakama ya ndizi – Ubungo14923
Mwembe chai  – Ubungo8614
Manzese Bakharesa – Ubungo426
Sehemu zilizotembelewa na idadi ya wananchi waliopewa mafunzo

Mafunzo haya yaliwalenga wanawake, vijana na wanaume wa rika mbali mbali, na uwakilishi ulikuwa ni kama ifuatavyo:-

Jumla ya wananchi waliofikiwa ni 82.  Sambamba na utoaji wa elimu pia Haki Maendeleo iligawa machapisho mbali mbali kama inavyoonekana katika jedwali hapa chini: –

EneoMachapisho
Buguruni  – Ilala56
Manzese Darajani, -Ubungo33
Soko la Mahakama ya ndizi – Ubungo88
Mwembe chai  – Ubungo33
Manzese Bakharesa – Ubungo26

 Wananchi wengi wamelalamikia suala la wale ambao wamejiandikisha sababu moja ama nyingine, mfano Ndugu Mwalusako wa manzese darajani alileleza kuwa yeye na madereva wenzake wa Magari ya Mizigo hawatakuwa na siku ya mapumziko kama wafanyakazi waklioajiriwa kwenye sekta rasmi, hivyo endapo atakuwa amepakia mzigo basi hatakuwa na nafasi ya kupiga kura ingawa amejiandikisha kwenye daftari na ana kadi yake.

Waendesha Boda boda ambao wengi ni vijana wakipewa elimu ya mpiga kura na vipeperushi

Pia Bi. Zainabu ambaye ni mfanyabiashara wa mboga mboga pia alieleza masikitiko yake kuwa yeye aliljiandikisha Mtwara na sasa anaishi Dar es Salaam na aliuliza kama anaweza kupiga kura siku ya uchaguzi, ingawa Tume ya uchaguzi ilitangaza na kufanya zoezi la kuhuisha(up-date) daftari la mpiga kuwa ila inaonekana mwitikio haukuwa wa kutosha au wananchi hawakuipa uzito suala hili.

Bwana Rajabu alikuwa anataka kujua suala zima la upigani kura, nani mambo gani ya kufuata, suala hili ambalo pia lipo katika machapisho mbali.

Katika kipindi hichi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge wa jamhuri ya muungano na madiwani wa Tanzania Bara, Haki Maendeleo inawakumbusha wapiga kura kutambua kuwa kuna “Haki na wajibu” wa mpiga kura kuwashauri washiriki kikamilifu kwenye mikutano ya wanasiasa wanaopita kuomba fursa za kuwawakilisha ni nini watafanya katika kuwaletea Maendeleo wananchi.

Haki Maendeleo (HM) ni Asasi isiyo ya kiserikali inayofanya kazi Tanzania Bara yenye namba za usajili Na. ooNGO/R/0274, kazi zetu ni kutoa elimu ya uraia, Haki za Binadamu pamoja na Utawala Bora.

Hatufungamani na, itikadi yoyote ile ya kisiasa, maslahi ya kiuchumi au dini na tunafadhiliwa zaidi na wanachama wetu na wafadhili wa umma.

Taasisi hii imechaguliwa na tume ya taifa ya uchaguzi kutoa elimu ya mpiga kura na kuwa waangalizi wa ndani wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

info@hmtanzania.or.tz

www.hmtanzania.or.tz

+255735461522